iqna

IQNA

al aqsa
Jinai za Israel
IQNA - Makumi ya walowezi wa Kizayuni wamevamia Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) siku ya Jumatatu chini ya ulinzi mkali wa wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel ambao unakalia eneo hilo kwa mabavu.
Habari ID: 3478720    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/23

Msikiti wa Al Aqsa
IQNA - Takriban waumini 125,000 wa Kipalestina walikusanyika katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa al-Quds (Jerusalem) kwa ajili ya sala ya tatu ya Ijumaa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani licha ya kuwekewa vikwazo vikali na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478604    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/30

Kadhia ya Palestina
IQNA - Wakati utawala haramu wa Israel umeweka vikwazo vya kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa al-Quds, zaidi ya waumini 100,000 wa Kipalestina walishiriki katika Swala maalum ya mwezi wa Ramadhani kwenye msikiti huo siku ya Ijumaa.
Habari ID: 3478560    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/23

Jinai za Wazayuni
IQNA - Lawama zimeongezeka baada ya utawala ghasibu wa Israel kuweka vizuizi katika milango mitatu ya kuelekea Msikiti wa Al-Aqsa katika eneo la Quds (Jerusalem) Mashariki linalokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3478516    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/15

Kadhia ya Palestina
IQNA - Utawala wa Kizayuni wa Israel unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina umetangaza siku ya Jumanne kwamba utawaruhusu waumini kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa katika eneo la Quds (Jerusalem) katika wiki ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani, na hivyo kutupilia mbali mpango wa awali wa kuweka vizuizi.
Habari ID: 3478461    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/06

Kadhia ya Al Aqsa
IQNA-Mkuu wa Ofisi ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewataka Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu Israel kuandamana hadi Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3478432    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/29

Jinai za Israel
IQNA - Kutakuwa na mlipuko na maafa makubwa hivi karibuni ikiwa utawala wa Kizayuni utaendelea na mpango wa kuwazuia Waislamu kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ilionya.
Habari ID: 3478412    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/25

Jinai za Israel
IQNA - Vikosi vya Israel vimewashambulia waumini karibu na lango la Asbat, lango kuu la kuingia Msikiti wa Al-Aqswa katika mji Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, wakiwazuia na kuwapiga walipokuwa wakijaribu kuingia msikitini humo kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3478401    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/23

Watetezi wa Palestina
IQNA-Mufti Mkuu wa Oman kwa mara nyingine amesisitiza umuhimu wa Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel na akasema kuukomboa ni jukumu la Waislamu wote duniani.
Habari ID: 3478232    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/22

Jinai za Israel
IQNA - Maelfu ya waumini wa Kiislamu walizuiliwa na jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) kwa ajili ya kuswali swala ya Ijumaa.
Habari ID: 3478216    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/19

Jinai za Israel
IQNA - Idara ya Wakfu ya Kiislamu, inayosimamia Msikiti wa Al-Aqsa huko al-Quds (Jerusalem), imesema leo kwamba ni waumini 15,000 pekee walioruhusiwa kuingia katika eneo hilo takatifu kwa ajili ya Sala ya Ijumaa kutokana na vikwazo vilivyowekwa na utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3478154    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/05

IQNA - Idara ya Waqfu ya Kiislamu huko al-Quds (Jerusalem) imesema kumeshuhudiwa ongezeko la idadi ya walowezi wa Kizayuni waliouhujumu Msikiti wa Al-Aqsa mwaka jana.
Habari ID: 3478133    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/02

Jinai za Israel
IQNA – Mji wa Al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel Ijumaa umeshuhudia vikosi vya Israel vikitumia gesi ya kutoa machozi na nguvu ziada kuwatawanya waumini karibu na eneo la Msikiti wa Al-Aqsa huku watu wengi wakiugua kwa kuvuta gesi hiyo ya machozi.
Habari ID: 3478072    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/22

Quds Tukufu
IQNA - Sheikh Ekrima Sabri, mhubiri wa Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem), aliitwa na mamlaka ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhojiwa siku ya Jumapili.
Habari ID: 3478052    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/18

Jinai za Israel
IQNA - Maelfu ya Wapalestina hawakuweza kuhudhuria sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) kwa wiki ya kumi kutokana na vizingiti vilivyowekwa na utawala dhalimu wa Israel tangu kuanza kwa vita dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7.
Habari ID: 3478040    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/16

Fatwa
CAIRO (IQNA) – Taasisi ya Dar ul Ifta ya Misri imetangaza kuwa hairuhusiwi au haijuzu kidini kuupa msikiti wowote jina la Al-Aqsa.
Habari ID: 3477955    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/28

Kadhia ya Palestina
AL-QUDS (IQNA) - Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa al-Quds (Jerusalem) ni mahali pa ibada kwa Waislamu peke yao na ni haki takatifu isiyopingika kwao, mkuu wa Kamati ya Juu ya Rais ya Masuala ya Kanisa huko Palestina alisema.
Habari ID: 3477628    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/20

Kadhia ya Palestina
Al QUDS (IQNA) - Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Ijumaa ya jana iliyosaliwa kwenye Msikiti wa Al-Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) licha ya kuwekewa vizuizi na kukabiliwa na hatua kali za kiusalama zilizochukuliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mji huo unaoukalia kwa mabavu.
Habari ID: 3477538    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/02

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Kundi la kutetea haki za binadamu limeonya kuhusu njama ya utawala ghasibu wa Israel kugeuza Jumba la Sala la Bab Al-Rahma katika Msikiti wa Al-Aqsa kuwa sinagogi.
Habari ID: 3476917    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/26

Ulimwengu wa Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali mashambulizi ya Wazayuni katika eneo la Babul Rahma katika Msikiti Mtakatifu wa al Aqsa.
Habari ID: 3476910    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/24